Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:33

Mkuu wa majeshi ya Libya ajiuzulu.


Waandamanaji wanaounga mkono serikali wakiandamana dhidi ya wanamgambo wenye silaha huko Tripoli, Libya, May 3, 2013.
Mkuu wa jeshi la Libya amejiuzulu baada ya mapigano kati ya waandamanaji na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali kupelekea kufariki kwa watu 31 katika mji wa mashariki wa Benghazi.

Ghasia zilizuka Jumamosi wakati waandamanaji mjini Benghazi walipovamia ngome ya kundi la wanamgambo wa kiislam wanaolipwa na serikali kusaidia kulinda usalama.

Waandamanaji hao walikuwa wanadai wanamgambo waweke silaha chini na kujisalimisha kwa maafisa wa majeshi ya Libya.

Mkuu wa majeshi ya Libya Youssef al Mangush ambaye alikuwa msimamizi wa wanamgambo alijiuzulu Jumapili. Mkuu huyo amekosolewa kwa kuchelewa kuunda jeshi la kitaifa na kuwaacha wanamgambo waongezeke.
XS
SM
MD
LG