Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:05

Rasimu ya katiba mpya ya Tanzania yatangazwa


Waandamanaji wanataka mageuzi ya katiba yafanyike Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Waandamanaji wanataka mageuzi ya katiba yafanyike Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Tanzania imeingia katika historia mpya Jumatatu baada ya kusomwa kwa rasimu ya awali ya katiba ya nchi hiyo iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba ikiwa imependekeza masuala kadhaa yatakayobadili muundo wa serikali ya nchi hiyo.

Miongoni mwa mambo makuu yaliyopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba katika rasimu hiyo ya awali ya katiba ni pamoja na kuwa na muungano wa serikali tatu, yaani ya Shirikisho, ya Tanznaia bara na Zanzibar huku mambo ya muungano yakipunguzwa kutoka 22 ya sasa hadi kubaki saba.

Aidha tume ya mabadiliko ya katiba imependekeza kuwa spika wa bunge na naibu wake asitoke kwenye wabunge au chama chochote cha siasa na pia kuweka ukomo wa mtu kuwa mbunge ambapo sasa itakuwa mwisho vipindi vitatu. Tume ya mabadiliko ya katiba pia imependekezwa kufutwa kwa wabunge wa viti maalum na wabunge wa muungano kuwa 75, 20 kutoka Zanzibar na 50 Tanzania bara huku watano watateuliwa na rais kutoka kundi la watu wenye ulemavu.

Ripoti ya Dinah Chahali - 2:53
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa upande wa tume ya uchaguzi. Tume ya mabadiliko ya katiba imependekeza tume kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi ambapo sifa za kuwa mjumbe wa tume hiyo huru ya uchaguzi zitaainishwa kwenye katiba na pia kuwa na kamati maalum ya uteuzi wa wajumbe. Majukumu ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa yataunganishwa kwenye tume huru ya uchaguzi

Tume ya mabadiliko ya katiba pia imependekeza kuruhusiwa mgombea binafsi kutoka ngazi ya chini hadi urais, hata hivyo imeacha umri wa miaka 40 kuwa ndio wa kuanzia mtu kuruhusiwa kugombea urais..Aidha wamependekeza mawaziri wa muungano wasizidi 15 na uteuzi wao utathibitishwa na bunge..

Jambo lingine kubwa walilopendekeza tume ya mabadiliko ya katiba kuwepo kwenye rasimu hiyo ya awali ya katiba ni pamoja na kuwa na haki ya kuhoji matokeo ya urais katika mahakama ya juu zaidi waliyopendekeza iwepo kwenye katiba, lakini kwa yule tu aliyegombea urais na kwamba mshindi wa urais atatangazwa iwapo atapata zaidi ya asilimi 50 ya kura zote.

Asha Rose Migiro naibu katibu mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa alizungumzia suala la mgombe binafsi na kutaka umakini utumike katika kujadili na hatimaye kufikia muafaka kutokana na unyeti wa suala lenyewe..

Peter Kuga Mziray aliwakalisha vyama vya siasa..katika uzinduzi huo wa rasimu ya awali ya katiba..na kupongeza tume ya mabadiliko ya katiba kuweka mambo kadhaa ambayo wapinzani walikuwa wakiyapigania ikwemo muunda wa muungano wa serikali tatu na suala la Rais kupata zaidi ya asilimia 50

Rasimu hii ya awali ya katiba ndiyo itakayojadiliwa na wajumbe wa mabaraza ya wilaya ya katiba baadaye mwezi huu hadi wa mwezi wa nane mwaka huu ambapo kupitia maoni ya mabaraza hayo, tume itakaa tena kuiboresha ili kupata rasimu kamili ya katiba mpya ambayo itapelekwa katika bunge la katiba kabla ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni mwaka 2014.
XS
SM
MD
LG