Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:40

Gazeti la Monitor laruhusiwa kuendelea na shughuli zake kwa masharti.


Waandishi wa gazeti la Monitor wakiwa wameziba midomo yao wakati wa maandamno kupinga kufungiwa huko Kampala, Uganda, May 20, 2013.
Waandishi wa gazeti la Monitor wakiwa wameziba midomo yao wakati wa maandamno kupinga kufungiwa huko Kampala, Uganda, May 20, 2013.
Mei 20 Polisi wa Uganda walizingira gazeti la Monitor mjini Kampala na kusema eneo hilo ni eneo la uhalifu , radio mbili shirika na gazeti hilo pamoja na gazeti jingine pia yalifungiwa .

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Maafisa wanasema walikuwa wanatafuta barua iliyoandikwa na Jenerali wa Uganda David Sejusa wa jeshi la Uganda akidai kuwa rais Yoweri Museveni ana mpango wa kumweka mwanaye kuwa rais baada ya yeye kuondoka, barua hiyo ilitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mipango ya kuuwa maafisa ambao inaelekea wanapinga mipango ya rais.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi waziri wa mambo ya ndani Hillary Oneck alisema kuzingirwa kwa gazeti la Monitor kumeondolewa baada ya wahariri wa gazeti hilo kukubali kutochapisha habari zinaoweza kuleta mvutano nchini humo, alisema pia kuwa utawala wa gazeti hilo unakiri kwamba kumekuwa na ukiukaji wa sera za kihariri.

Mwandishi mwandamizi wa Monitor Tabu Butigira alitetea utendaji kazi wa gazeti hilo akiiambia sauti ya Amerika kuwa malalamiko ya serikali hayakuwa kuhusu ukweli wa habari yenyewe isipokuwa kilichomo ndani yake.

Jumanne Polisi walitumia mabomu ya machozi na kukamata waandishi kadhaa waliokuwa wakiandamana nje ya ofisi za Monitor, rais Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu 1986 anatazamiwa kuachia madaraka 2016, hajasema chochote kuhusu atakayechukua nafasi yake lakini wengi wamekuwa wakinong’ona kuwa kupanda haraka kwa mwanawe katika ngazi za kijeshi inawezekana ni dalili ya kwamba anamtayarisha kwa nafasi hiyo.
XS
SM
MD
LG