Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:01

Rais Omar al Bashir atishia kufunga bomba la mafuta.


Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akizungumza na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.
Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir akizungumza na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.
Rais wa Sudan Omar al Bashir anatishia kufunga bomba linalobeba mafuta kutoka Sudan Kusini kwenda kaskazini , anasema kusini inaunga mkono waasi.

Bw.Bashir alisema katika hotuba ya Televisheni Jumatatu kwamba Sudan itafunga bomba hilo la mafuta, kama Sudan Kusini itawapa uungaji mkono wa aina yeyote waasi, katika maeneo ya mpakani ya Kordofan Kusini na Blue Nile na eneo lenye utete mkubwa la magharibi la Darfur.

Rais huyo akilindwa na maafisa wa jeshi, alizungumza baada ya jeshi kusema limechukua tena mji wa Abou Kershola kutoka kwa waasi huko Kordofan Kusini.
XS
SM
MD
LG