Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 11:52

Afrika yaadhimisha miaka 50 OAU


Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria (R) na mwenzake rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania kwenye kikao cha kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika. Addis Ababa May 25, 2013.
Viongozi wa mataifa 52 wanachama wa Umoja wa Afrika AU wameanza sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Jumuia ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, OAU, iliyosaidia mataifa ya kiafrika kujikombowa kutoka mataifa ya kikoloni na ambayo hivi sasa yanajaribu kutokomeza umaskini na migogoro barani humo.

Akifungua mkutano wa viongozi wa AU mjini Addis Ababa siku ya Jumamosi, waziri mkuu wa Ethopia Hailemariam Desalegn amesema malengo ya awali ya umoja huo yangali yanafaa kuleta muungano wa Afrika.

Amewahimiza viongozi wa Afrika kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanatokomeza umsakini na kumaliza migogoro katika bara hilo.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry ambae ni miongoni mwa wageni wa heshima wanaohudhuria sherehe hizo, kabla ya kufunguliwa mkutano amesema, Nigeria inahaki ya kujilinda kutokana na magaidi, lakini alieleza wasi wasi juu ya uwezekano wa ukiukaji wa haki za binadam unaofanywa na wanajeshi wa serikali katika juhudi za kuwaangamiza magaidi hao.

Viongozi hao wa Afrika wanatarajiwa pia kujadili pendekezo la serikali ya Kenya kuitaka AU kuwasilisha pendekezo mbele ya Baraza la Usalama kulitaka baraza kuruhusu kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto inaondolewa mbele ya mahakama ya ICC na kufanyika huko Kenya.
Mjadala juu ya miaka 50 ya AU
please wait

No media source currently available

0:00 0:17:39 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika kipindi cha "Live Talk", cha Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Balozi wa Umoja wa Marika Marekani Bi. Amina salum Ali, na Mwalimu Bashiru Ally mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam wamezungumzia historia, changamoto na matarajio ya Umoja huo miaka 50 ijayo.
XS
SM
MD
LG