Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:27

Katibu mkuu UN na Russia wazungumzia Syria.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon (kushioto) na rais Vladimir Putin wa Rashia wakizungumza baada ya kukutana ikulu ya Bocharov Ruchei kwenye bahari ya Black Sea Sochi, May 17, 2013.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon (kushioto) na rais Vladimir Putin wa Rashia wakizungumza baada ya kukutana ikulu ya Bocharov Ruchei kwenye bahari ya Black Sea Sochi, May 17, 2013.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon yuko Russia ambako amesema ni muhimu kutopoteza kasi katika mazungumzo ya kuandaa mkutano wa amani juu ya Syria mwezi ujao.

Bw.Ban aliwaambia waandishi wa habari maendeleo yaliyopatikana katika mazungumzo ya hivi karibuni kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov lazima yafanyiwe kazi, badala ya kuyaacha yapotee.

Amesema timu ya Umoja wa mataifa iko tayari wakati wowote kuchunguza madai kwamba serikali ya rais Bashar Al Assad ilitumia silaha za sumu dhidi ya waasi.

Bw.Ban yuko katika mji wa mapumziko wa Sochi ulioko Black Sea kukutana na rais wa Russia Vladmir Putin kwa mazungumzo kuhusu Syria.
XS
SM
MD
LG