Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:58

Nawaz Sharrif anaongoza katika uchaguzi wa Pakistan.


Waziri mkuu ajaye Pakistan Nawaz Sharrif akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Raiwind.
Waziri mkuu ajaye Pakistan Nawaz Sharrif akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Raiwind.
Matokeo ya awali yasiyo rasmi katika uchaguzi wa kihistoria wa bunge nchini Pakistan yanaonesha mwanasiasa mkongwe na waziri mkuu mara mbili Nawaz Sharif atapata ushindi na kuiongoza tena nchi hiyo.

Wapakistani wanamatumiani makubwa kwamba serikali mpya itaweza kutanzua matatizo mengi ya kiuchumi na usalama ya nchi hiyo

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anasema licha ya vitisho wapigaji kura wamejitokeza kwa wingi ikiwa ni ishara kwamba wananchi wanataka mabadiliko na kutaka sauti zao zisikike.

Mchambuzi wa kisiasa Raza Rumi anasema jinsi serikali mpya itakavyoweza kufanya kazi kwa bidi itategemea ni aina gani ya muungano Nawaz sharif na chama chake wataweza kuunda.

“Ushindi wa Nawaz Sharif ni mkubwa kabisa katika jimbo anakotoka lakini bila shaka atahitaji uungaji mkono kutoka majimbo mengine madogo na inabidi afikie maridhiano juu ya masuala matatu muhimu yanayoikumba Pakistan, kwanza mzozo wa uchumi na nishati, siasa kali na uwanaharakati wa kutumia nguvu ulovuruga amani ya Pakistan, tatu na muhimu zaidi kuendelea na sera ya ushirikiano na India kunufaika na mapato ya biashara .

Licha ya kuwepo na ghasia nyingi kabla ya uchaguzi wapiga kura walijitokeza kwa wingi. Na matokeo yakiwa yanatolewa mchazaji maarufu wa zamani wa mchezo wa kriket Imran Khan na chama chake cha Tehreeke-e-Insaf PTT, kiliwashangaza wengi kuchukua nafasi ya pili ikiwa ni mara ya kwanza kujingiza katika siasa. Wafuasi wake walikuwa na furaha kupita kiasi. Waseem Shahzad anasema ujumbe wa Khan wa kuleta mageuzi uliwahamasisha wengi.
XS
SM
MD
LG