Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 05:06

Jenerali wa Uganda amshutumu Museveni kutaka kumwachia madaraka mwanae.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Jenerali mmoja wa jeshi anamshutumu rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kujaribu kuhakikisha mwanae anarithi madaraka kama kiongozi wa nchi hiyo, akiwa ni kiongozi wa kwanza wa juu kuelezea wasi wasi wake juu ya mpango wa mrithi wa madaraka wa rais Museveni baada kuwepo madarakani kwa karibu miongo mitatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP , David Sejusa mmoja wa majenerali 6 wa Uganda alisema katika barua yake ya hivi karibuni kwa mkuu wa usalama wa taifa kwamba anataka uchunguzi ufanyike juu ya shutuma kwamba wale watakaompinga mtoto wa museveni kuwa kiongozi ajaye wanaweza kulengwa kuuwawa.

Jenerali Nyaronda Nyaikirima kamanda wa juu wa jeshi alisema Jumanne kwamba jeshi limedahalilishwa na barua ya Sejusa.

Shutuma hizo na afisa wa juu wa jeshi zimewashtua wengi huko Uganda.
XS
SM
MD
LG