Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:58

Wafanyakazi wa Korea Kusini warudi nyumbani kutoka Kaesong.


Waandishi wa habari wakisubiri raia wa Korea kusini wanaorudi nyumbani kutoka kutoka kiwanda cha Kaesong Korea kaskazini.
Waandishi wa habari wakisubiri raia wa Korea kusini wanaorudi nyumbani kutoka kutoka kiwanda cha Kaesong Korea kaskazini.
Korea Kusini inasema kurudi kwa wafanyakazi wake waliobaki kwenye eneo la kiwanda inachokiendesha ikishirikiana na Korea Kaskazini kumecheleshwa kwa kile ilichokiita taratibu za dakika za mwisho za kiutawala.

Msemaji wa wizara ya muungano ya Korea Kusini aliiambia VOA kwamba Kaskazini na Kusini wanamalizia mazungumzo ya mwisho ya ushauri juu ya masuala ya utendaji kuhusiana na eneo la kiwanda cha Kaesong. Hatua hiyo itavunja mahusiano ya mwisho ya amani kati ya wapinzani hao wa rasi ya Korea.

Wafanyakazi 50 waliobaki kwenye kiwanda hicho walitarajiwa kurudi nyumbani jumatatu. Seoul ilitangaza inarudisha raia wake nyumbani kutoka kiwanda cha Kaesong baada ya Pyongyang kukataa ombi la mazungumzo ya kurejesha shughuli katika kiwanda hicho.
XS
SM
MD
LG