Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 16:47

Mapigano Nigeria yapelekea vifo 187.


Wakazi wakiangalia gari lililolipuliwa baada ya mlipuko huko Maiduguri.
Dazeni ya watu wameuwawa kaskazini mwa Nigeria katika mapigano makali kati ya wanamgambo wa kiislam na majeshi ya serikali.

Afisa wa eneo hilo Lawan Kole amesema watu 187 wameuwawa ingawa shirika la habari la AFP limemkariri msemaji wa kijeshi kwamba idadi hiyo imeongezwa.

Mapigano hayo yalianza Ijumaa katika kijiji cha Baga , yakilazimisha maelfu ya wakazi kukimbia eneo hilo.

Wakazi wa eneo hilo wanasema mapigano yalianza baada ya vikosi vya jeshi kuzingira msikiti huo ambao ulikuwa unashutumiwa kwa kuhifadhi wanachama wa kundi la Boko Haram .
XS
SM
MD
LG