Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:53

Msako mkali Boston kwa mshukiwa ulipuaji mabomu.


Msako unaendelea kwa mshukiwa wa pili.
Msako unaendelea kwa mshukiwa wa pili.
Polisi katika jimbo la Massachusetts wanaendelea na msako mkali wa mmoja wa washukiwa wa mabomu ya Jumatatu katika mji wa Boston baada ya kumuuwa mwingine katika majibizano ya risasi Alhamisi usiku. Vyombo vya habari Marekani vinaripoti kuwa washukiwa hao ni ndugu wenye asili ya Chechnya.

Maafisa wanasema mshukiwa aliyekuwa amevaa kofia nyeupe kwenye milipuko ya kwenye mashindano ya riadha, ajulikanaye kama mshukiwa namba mbili hajulikani alipo na anaripotiwa kuwa hatari na mwenye silaha. Polisi wanawaasa wakazi wa Watertown kiasi cha kilometa 8 kutoka Boston, wakae ndani na wasifungue milango yao kwa mtu yeyote isipokuwa Polisi. Polisi wanakwenda nyumba hadi nyumba kumtafuta mshukiwa huyo.
Shirika la habari la NBC linaripoti kuwa washukiwa hao wawili ni ni ndugu, mtu na kaka yake wenye asili ya Chechnya. Shirika la AP linasema wanatoka kwenye jimbo moja karibu na Chechnya.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndugu hao walikuwa wakiishi Marekani kihalali na mshukiwa ambaye anatafutwa sasa ni Dzhokar Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19.

Maafisa wanasema mshukiwa mmoja aliyepigwa picha na FBI akiwa na kofia nyeusi alijeruhiwa vibaya na risasi Alhamisi usiku na kufariki baada ya kupelekwa hospitali. Mshukiwa alikuwa akirusha vifaa vya milipuko wakati akijaribu kukimbia.
XS
SM
MD
LG