Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 08:47

Maddona ashutumiwa na Malawi kutosema ukweli


Madonna akiwa na mtoto aliyemchukua kumlea kutoka Malawi (Foto AFP)
Serikali ya Malawi imemshutumu muimbaji mashuhuri Maddona kwa kutia chumvi kuhusu kazi yake ya msaada wa kibinadamu nchini humo na kutaka kupewa huduma maalum wakati wa ziara yake nchini humo wiki iliyopita.

Taarifa kutoka ofisi ya rais Alhamisi imesema Maddona anataka Malawi iendelee kukaa kwenye kifungo cha kumshukuru kwa sababu amechukua kulea watoto wawili wa Malawi.

Taarifa hiyo imeendelea kutaka kujua nia ya dhati ya kazi yake hiyo ya kusaidia na kusema kwamba muimbaji huyo inabidi ajifunze thamani ya kusema ukweli. Taarifa hiyo imesema amechangia ujenzi wa madarasa na sio kujenga shule kama ilivyodaiwa .

Madonna naye kwa upande wake amesema amesikitishwa na rais wa Malawi Joyce Banda ambaye amechagua kudanganya juu ya kazi zake za misaada , nia yake na jinsi alivyofanya wakati alipokuwa nchini humo.

Taarifa kwenye mtandao wake wa Raising Malawi inasema Madonna hapo awali alitaka kujenga shule ya wasichana lakini akagundua kwamba lengo lenye maendeleo zaidi litakuwa ni kujenga shule ndogo ndogo katika vijiji nchini kote.
Maddona anasema kutokukubaliana kwao kumetokana na kufukuzwa kazi kwa dada wa rais Banda , Anjimile Oponyo ambaye alifanya kazi kama mkuu wa taasisi hiyo ya misaada. Oponyo alifukuzwa kazi kufuatia shutuma za matumizi mabaya ya dola milioni 3.8 za misaada.

Oponyo anashitaki taasisi hiyo kwa kumfukuza kazi kimakosa.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG