Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:02

Serikali ya Mapinduzi C.A.R yatangaza serikali ya mpito


Wapiganaji wa kundi la waasi la Seleke wapiga doria kati kati ya mji mkuu wa Bangui. March 27, 2013.
Wapiganaji wa kundi la waasi la Seleke wapiga doria kati kati ya mji mkuu wa Bangui. March 27, 2013.
Kiongozi wa mapinduzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema atashika nyadhifa mbili urais na waziri wa ulinzi.

Michel Djotodia ambaye jeshi lake la uasi lilimpindua rais Francois Bozize ametoa tangazo hilo katika taarifa iliyosomwa kwenye radio ya taifa jumapili jioni.

Wanachama wake wa kundi la uasi la Seleka watashika nafasi za mawaziri katika wizara mbalimbali.

Nicolas Tiangae kiongozi wa upinzani aliyejiunga na serikali ya zamani kama sehemu ya ushirikiano wa madaraka bado atabaki kuwa waziri mkuu.
Umoja wa afrika iliondoa C.A.R katika jumuiya yake na kupinga harakati zake za hivi karibuni.

Mjini Washington msemaji wa wizara ya mambo ya nje Victoria Nuland anasema uongozi ulikuwa na wasiwasi kwamba waasi watachukua hatua dhidi ya serikali ambayo kwa maneno yake anasema haikuwa ya kidemokrasia wala iliyo wazi.

Nchi hiyo ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ina historia ya matukio ya mapinduzi tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka 1960.

Miongoni kadhaa ya mizozo na kutokuwa na utawala bora vimesababisha watu wa nchi hiyo kubaki masikini , licha ya kuwa na hifadhi kubwa na madini ya dhahabu na almasi.
XS
SM
MD
LG