Papa Francis ameombea kuwepo na amani duniani katika ujumbe wake wa kwanza wa Pasaka alioutoa kwenye kibaraza cha kanisa la St.Peter.
Akihutubia umati wa watu wapatao 250,000 kutoka pembe mbali mbali za duniani, mkuu huyo wa kanisa la katoliki aliombea hasa maridhiano katika sehemu zenye ghasia ikiwa ni pamoja na eneo la rasi ya Korea , Mali, Nigeria na mashariki ya kati.
Wakristo duniani kote walisheherekea Pasaka Jumapili. Ni siku takatifu katika mwaka wa liturjia ya kanisa ambao unaadhimisha kufufuka kwa muokozi wao Yesu Kristo.