Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 14:12

Yatima wa mauaji ya halaiki Rwanda wahitimu masomo ya sekondari.


Mtoto yatima akiwa kabebwa.
Mtoto yatima akiwa kabebwa.
Heyman ni wakili aliyezaliwa Afrika kusini , ambaye sasa anaishi New York aliona tatizo la yatima huko Rwanda na kutaka kusaidia wale waliokuwa yatima wakati na baada ya mauaji ya halaiki, na kwa ajili yao alibuni kijiji cha vijana ambapo zaidi ya vijana 100 wa shule za sekondari, waliohitimu shule ya sekondari na kufaulu kitaifa wanahudumiwa.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Joe De Capua anaripoti mafanikio hayo muhimu na kazi nzuri katika kijiji hicho cha vijana kinachojulikana kama Agahazo –Shalom Youth Village. Jina hilo ni muungano wa Kinyarwanda na Kiyahudi Agahozo ina maana ya pale machozi yamekauka na Shalom ikiwa na maana ya amani.
please wait

No media source currently available

0:00 0:07:17 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kijiji cha vijana cha Agahozo Shalom kiko kiasi cha saa moja kwa gari mashariki mwa Kigali karibu na mji wa Rwamagana. Kimejengwa kwenye shamba ambalo Heywood na waunga mkono walinu kutoka kwa wamiliki ardhi wa eneo hilo.

Ni shule ya sekondari ya Liqudent Family, ambapo wote isipokuwa mwanafunzi mmoja kati ya 118 walofaulu mtihani wa kitaifa wa Rwanda miezi michache iliyopita.

Ni wanafunzi wa kwanza waliohitimu katika shule hiyo na hivi sasa wanasubiri kuona nani atagharimia au kuwapatia mkopo wa kuweza kuendelea na masomo ya juu. Na wale ambao hawatabahatika itabidi wacheleweshe masomo ya juu hadi kupata kazi na kuweka kando fedha kuweza kuendelea na masomo.

Kwa wastani familia ni ya vijana 16 pamoja na wale waitwao kaka au dada, ambao wanafanya kazi katika kijiji, na kila familia inaongozwa na mama.

Kila usiku kuna wakati wa familia .Kwa kiasi cha saa moja jamii ya kila familia wanakutana pamoja kuzungumzia matukio ya siku hiyo , masuala kijijini au taarifa mpya kuhusu masuala nyeti.

Pia kuna madarasa juu mbinu za kazi kama kuandika juu ya ujuzi wako wa kazi au kufanya mahojiano na madarasa juu ya huudma , kompyuta na kilimo cha kisasa.
Heyman anasema fedha za kugharimia kazi hizo zote zinapatikana kwa kiasi kikubwa kutoka kwa michango na muda mwingi unatumika kutafuta msaada.

Anatarajia siku moja kugeuza Agahozo Shalom kuwa kijiji kinchojitegemea , ambapo biashara ndogo ndogo zitaweza kuendesha operesheni.

Kijiji cha vijana cha Agahozo Shalom kina taarifa ya filosofia . Inasema kwa upande kila vijana aliyeteseka ana maisha yaliyopita, ya sasa na siku za mbele. Heyman anasema maisha kijini hapo ni juu ya kujenga upya.
XS
SM
MD
LG