Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:54

Waziri mkuu wa Ireland na Meya wa Newyork waongoza gwaride la siku ya Mt.Patrick


Gwaride la siku ya Mt.Patrick.
Gwaride la siku ya Mt.Patrick.
Maelfu ya watu nchini kote Ireland na Marekani wamesheherekea sikukuu ya Mt.Patrick Jumapili kwa magwaride na kwenye maeneo ya starehe.

Huko Dublin Ireland makundi yanayokadiriwa kufika maelfu ya watu yalipambana na baridi kali ili kushiriki katika sherehe hizo za kila mwaka ambazo zilianza kwa gwaride la kitamaduni.

Wakati akiwa Newyork waziri mkuu wa Ireland Enda Kenny aliungana na Meya Michael Blomberg katika kuongoza gwaride hilo la mwaka la wachezaji na mashirika ya kiraia na kitamaduni ya Ireland .

Kwingineko duniani darzeni ya majengo makuu ya alama ikiwa ni pamoja na Mapyramid ya Misri na lile la Barazil la Christ the Redeemer yalijazwa taa za kijani kwa heshima ya siku ya Mt. Patrick.
XS
SM
MD
LG