Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 13:56

Jeshi la Polisi Uganda kushitakiwa ICC.


Kiiza Besigye kiongozi wa zamani wa upinzani wa chama cha FDC.

Aliyekuwa rais wa chama cha upinzani cha FDC daktari Kiiza Besigye, anasema akishirikiana na wanaharakati wengine wa mapinduzi wajulikanao kama 4GC yaani For God and my country, wamo kwenye harakati za kukusanya ushahidi wa kutosha ili waweze kulishtaki jeshi la polisi la Uganda kwenye mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC.

Wiki chache zilizopita, Daktari Kiiza Besigye akishirikiana na meya wa Kampala Erias Lukwago walikamatwa na polisi walipokuwa wanajaribu kufagia kwenye mtaa mmoja hapa mjini Kampala. Polisi ilisema kufagia kwao kulikuwa kisingizio tu wakidai kuwa lengo lao lilikuwa kuwakusanya watu na kisha kuzua vurugu mjini.

Akizungumza na waandishi habari mjini Kampala, Besigye alionyesha picha za polisi na watu wengine wakiwa wamevalia nguo za kiraia walimpiga dereva wake pamoja na wafuasi wake.

polisi imekuwa ikiwakusanya vijana na kuwapa mafunzo ya kijeshi ili wawapige wanasiasa wanaoupinga uongozi wa rais Museveni. Kikundi anachokizungumzia kinaitwa voice of movement youth.

Besigye anasema wao kama wanaharakati wa mapinduzi hawataketi tu na kuangalia polisi ikitumia vibaya nguvu zake.

Msemaji wa polisi Judith Nabakooba aliyakana madai ya 4GC kuwa wanashirikiana na makundi yoyote. Alisema vijana waliozua fujo walikuwa baadhi ya vijana waliokuwa miongoni mwa wafuasi wa Besigye na polisi iliingililia kati wakati vita kati ya vijana hawa vilipozidi.

Mwaka wa 2011 kundi la 4GC lilijulikana kama activists for change na lilisifika kwa kuongoza maandamano ya kutembea kwenda kazini kupinga ongezeko la bei ya bidhaa nchini Uganda.
XS
SM
MD
LG