Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:50

Uchaguzi wa baba mtakatifu waendelea Vatican.


Makadinali wakiingia katika kanisa la Sistene mjini Vatican.
Makadinali wakiingia katika kanisa la Sistene mjini Vatican.
Moshi mweusi umetoka katika bomba dogo katika paa la kanisa dogo la Sistene katika mji wa Vatican, ikimaanisha Makadinali wa kanisa la Roman Katoliki wanaendelea kupiga kura kumtafuta baba mtakatifu mpya.

Makadinali 115 wanamtafuta mrithi wa kiti cha baba mtakatibu Benedict mwenye umri wa miaka 85 aliyejiuzulu mwezi wa pili akisema kuwa hana nguvu kiafya kuendelea na kazi za upapa.

Jopo la Makadilani limeanza siku ya pili jumatano ya kutafakari baada ya kipindi cha sala.

Maelfu ya watu wamekusanyika nje ya uwanja mkubwa wa St. Perte’s kusubiri ishara ya moshi mweusi au mweupe kuashiria kama amepatikana baba mtakatifu mpya.

Mara makadinali watakapokubaliana juu ya mrithi wa kiti hicho, moshi mweupe utatoka kwenye bomba dogo na kengele ya St. Peter’s Basilica italia.

Makadinali ni lazima wapate theluthi mbili ya kura ambayo ni sawa na kura 77 ya walio wengi kumchagua baba mtakatifu atakayeongoza kanisa katoliki.
XS
SM
MD
LG