Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:15

Mkutano wa makardinali kumchagua Papa mpya waanza


Enela kibaraza katika kanisa la Mt. Petro ambapo Papa mpya ataonekana kwa mara ya kwanza.
Enela kibaraza katika kanisa la Mt. Petro ambapo Papa mpya ataonekana kwa mara ya kwanza.
Macho na masikio ya wakatoliki yanaelekea Vatikan ambapo makardinali 115 wanaanza kumchagua Papa mpya Jumanne.

Mkutano wa makardinali utafanyika kwa faragha katika kanisa la Sistine na hautamalizika mpaka Papa mpya atakapopatikana . Hakuna anayesema ni muda gani utachukua . Lakini dunia itajua wakati kanisa litakapokuwa na kiongozi mpya wakati moshi mweupe utakapotoka kwenye sehemu maalum ya kutoa moshi uliowekwa kwenye dari ya kanisa hilo.

Atakayechaguliwa lazima apate kura 77 theluthi mbili ya walio wengi. Hakuna anayeongoza moja kwa moja katika nafasi hiyo kwa sasa.

Wakati kanisa katoliki linachagua Papa mpya , linafuata utaratibu ambao umekuwepo bila ya kubadilika kwa karne nyingi. Tofauti pekee safari hii ni kwamba Papa aliyepita Benedict XVI bado yuko hai.

Katika jioni ya kwanza kura ya kwanza itapigwa baada ya hapo watapiga kura nne kila siku, mbili asubuhi na mbili jioni. Mgombea atakayefanikiwa anahitaji theluthi mbili ya kura zilizopigwa.
XS
SM
MD
LG