Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:13

Mandela atoka hospitali.


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiwa nyumbani kwake.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiwa nyumbani kwake.
Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambaye ni alama kuu ya amani amerudi kwenye nyumba yake ya Johannesburg kufuatia vipimo vyake vya afya vilivyotoa matokeo mazuri katika hospitali moja ya Pretoria. Alilazwa siku moja iliyopita kwa ajili ya vipimo vya afya yake.

Rais wa Afrika Kusini alisema Jumapili kwamba madaktari wamekamilisha vipimo vyote vilivyokuwa vimepangwa na kwamba Bw.Mandela yupo kwenye hali nzuri na kama hapo siku za nyuma afya yake inaendelea kuangaliwa na timu ya madaktari.

Msemaji wa rais Mac Maharaj amesema hakuna sababu yeyote ya kuwa na wasi wasi wakati madaktari wakiendelea kumfanyia vipimo mshindi huyo wa nishani ya nobel mwenye umri wa miaka 94 na rais wa zamani. Bw.Mandela alilazwa mwezi Desemba kwa ambukizo kwenye mapafu.
XS
SM
MD
LG