Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:33

Venezuela kufanya uchaguzi wa Rais Aprili 14.


Mkuu wa tume ya uchaguzi ya venezuela Tibisay Lucena akitangaza tarehe ya uchaguzi wa urais wa nchi hiyo.
Mkuu wa tume ya uchaguzi ya venezuela Tibisay Lucena akitangaza tarehe ya uchaguzi wa urais wa nchi hiyo.
Vyama vya kisiasa vya Venezuela vinajiandaa kufanya kampeni za uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika aprili 14 kuziba nafasi ya rais Hugo Chaves kiongozi wa kisoshalisti aliyefariki wiki iliyopita baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

Tarehe ya uchaguzi ilitangazwa na tume ya uchaguzi ya Venezuela Jumamosi, siku moja baada ya makamu wa raia wa Chaves na mrithi aliyechaguliwa Nicolas Maduro kuapishwa kuwa kaimu rais wa nchi.

Maduro anatarajiwa kupambana katika uchaguzi huo na kiongozi wa upinzani Henrique Capriles gavana wa jimbo la Miranda aliyeshindwa na Chaves katika uchaguzi wa urais Octoba mwaka jana.

Capriles alipinga sherehe za kuapishwa kwa Maduro ijumaa akidai ni tukio linalopinga katiba.

Marais 18 wa Latino Amerika na viongozi wengine wa kigeni walihudhuria mazishi ya Chaves ambapo Marekani ilituma ujumbe wa kidiplomasia.
XS
SM
MD
LG