Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 10:25

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania ajeruhiwa vibaya.


Katibu Mkuu wa chama cha waandishi habari Tanzania Neville Meena akizungumza na waandishi habari.

Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa mara nyingine imetingishwa baada ya mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini humo, Absalom Kibanda kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jumatano nje kidogo ya jiji la dara es salaam.

Kibanda tayari amesafirishwa jioni hii kwa ndege maalum kwenda nchini Afrika kusini kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mujibu wa taarifa za awali za kitabibu , amejeruhiwa kichwani ambako alipigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni nondo. Jicho lake la upande wa kushoto limeathirika kwa kudhaniwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kucha katika kidole cha mkono wa kulia kung’olewa na meno mawili kung’olewa pia huku washambuliaji wakiwa hawajaondoka na kitu chochote.

Tukio la kujeruhiwa mweyekiti Kibanda limekumbusha tukio zito lililowahi kutoke akatika tasnia ya habati nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka jana baada ya mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha channel ten kuuwawa katika mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkioani Iringa

Neville Meena ni katibu mkuu wa jukwaa la wahariri amekemea kuhusu tukio hilo akisema kuwa linatishia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa uhuru.

Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako Kibanda alikuwepo kabla ya kusafirishwa kwa matibabu, nje ya nchi viongozi mbalimbali wa serikali vyombo vya habari na wanasiasa walifika kumjulia hali akiwemo bwana Reginald Mengi ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari Tanznania, MOAT.

Bwana Kibadna ambaye kwa sasa ni mhariri mtendaji mkuu wa kampuni ya New Habari inayomiliki magazeti kadhaa hapa nchini miezi michache iliyopita alikuwa mhariri mtendaji katika gazeti la Tanzania daima linalomilikiwa na familia ya mwenyekiti wa chama cha demokrasai na maendeleo CHADEMA, bwana Freeman Mbowe.

Mkurugenzi wa idara ya habari, maelezo hapa nchini Bwana Assah Mwambene alikuwepo pia hospitalini muhimbili.

Kamanda wa kanda maalum Suleimano Kova katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema kwa kushirikiana makao makuu ya polisi wameunda jopo la wapelelezi kumi kwa ajili ya kuchunguza kuvamiwa na kushambuliwa na hatimaye kujeruhiwa kwa mwenyekiti huyo wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda ambapo amekiri kwamba vitendo vya mashambulizi yanayoonekana ya kulipiza kisasi vimeshamiri kwa sasa.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dakta Gharib Bilal naye alikuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu aliyefika kumjulia hali bwan Kibada akiwa muhimbili kabla ya kusafirishwa nchini Afrika Kusini.
XS
SM
MD
LG