Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:12

Uhuru Kenyatta aongoza katika matokeo ya awali ya kura ya rais.


Mgombea urais wa Jubilee Uhuru Kenyatta akipiga kura katika jimbo lake la uchaguzi Gatundu , Kenya, March 4, 2013. (J. Craig/VOA)
Mgombea urais wa Jubilee Uhuru Kenyatta akipiga kura katika jimbo lake la uchaguzi Gatundu , Kenya, March 4, 2013. (J. Craig/VOA)
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta akiongoza katika kura ya rais.

Huku asilimia ya 10 ya vituo vya kupigia vikiwa vimeleta ripoti, Bw.Kenyatta anaongoza dhidi ya mpinzani wake mkuu raila odinga kwa asilimia 56 kwa 40.

Bw.Kenyatta ambaye alikuwa naibu waziri mkuu anakabiliwa na mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa tuhuma za kusaidia kupanga ghasia za kikabila za baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2007 .

Zaidi ya watu 1,100 waliuwawa katika ghasia hizo. Uchaguzi wa jana Jumatatu nchini Kenya ulikuwa kwa kiasi kikubwa wa amani ingawa saa chache kabla ya upigaji kura watu wapatao 13 ikiwa ni pamoja na maafisa 7 wa polisi waliuwawa kwenye pwani ya Kenya.
XS
SM
MD
LG