Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:10

Majeshi ya Ufaransa yapambana na wanamgambo wa kiislam huko Gao.


Kifaru cha Ufaransa kikisindikiza msafara wa majeshi huko Gao, kaskazini mwa Mali.
Kifaru cha Ufaransa kikisindikiza msafara wa majeshi huko Gao, kaskazini mwa Mali.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa anasema majeshi ya Mali na Ufaransa yamesukuma nje waasi wa kiislam ambao walichukua kwa muda mfupi manispaa ya mji huo na nyumba ya Meya katika mji wa Gao kaskazini mwa Mali.

Jean Yves Le Drian aliwaambia waandishi wa habari alhamisi mjini Brussels kwamba wanamgambo watano wa kiislamu waliuwawa katika mapigano na hali imerudi kuwa ya kawaida.

Mapigano mapya kati ya wanamgambo na majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na Ufaransa yalizuka jumatano mjini Gao,ambao ulichukuliwa tena na majeshi ya Ufaransa na Mali mwezi uliopita baada ya ukaliaji mabavu wa waasi wa kiislamu. Ripoti zinasema wanamgambo waislam wamerudi Gao usiku na kuchukua udhibiti wa baadhi ya majengo ya serikali.
XS
SM
MD
LG