Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 18:47

Kamati ya bunge kuchunguza mzozo wa gesi Mtwara.Bunge la Tanzania limeunda kamati maalumu ya wabunge watakaokwenda mikoa ya kusini Mtwara na Lindi kutathmini mzozo wa gesi katika mikoa hiyo.

Spika wa bunge Anne Makinda amesema kamati hiyo itarejesha matokeo yatakayopatikana na baadae kujadiliwa katika baraza la bunge lililoanza Jumatatu.
Wakazi wa mtwara wanapinga Serikali ya Tanzania kutumia bomba kusafirisha gesi iliyogundulika mkoani humo kwenda Dar es salaam hali iliyozua ghasia na kusababisha maafa ya watu.

Hadi sasa Serikali ya Tanzania imesisitiza kuendelea na msimamo wake wa kusafirisha gesi hiyo . Tayari kuna vikao kadhaa vimefanywa ili kuona jinsi ya kutatua mzozo huo lakini hakuna mafanikio yoyote.

Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari vya Tanzania akisema kuwa kama kila mkoa utagomea rasilimali zake basi nchi itapasuka vipandevipande hali iliyochechea tafrani.

Ona maoni (1)

mjadala huu umefungwa

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG