Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 21:21

Hali ya utulivu yarejea huko Eritrea.


Rais wa Eritrea Isaias Afewerki
Hali ya utulivu yaripotiwa kurejea tena huko Eritrea siku moja baada ya kundi la askari waasi kujaribu kuchukua wizara ya mambo ya habari ya nchi hiyo.
Zaidi ya askari waasi 100 walivamia wizara hiyo huko Asmara mapema Jumatatu na kuwaamrisha watangazaji wa habari wa Televisheni ya kitaifa kusoma taarifa ya kudai kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kusema katiba ya 1997 itaheshimiwa.
Haikujulikana mara moja jinsi gani hali hiyo ilivyotulizwa lakini wanajeshi hao inaaminika waliondoka wizarani hapo Jumatatu usiku.
Katika ujumbe uliotolewa kwenye mtandao wa Twitter Jumanne mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Eritrea Yemane Ghebremeskel amesema hali sasa ni tulivu.
XS
SM
MD
LG