Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:30

Vuguvugu la MRC labadili msimamo.


Katikati ni kiongozi wa MRC Omar Mwamnuadzi.
Katikati ni kiongozi wa MRC Omar Mwamnuadzi.
Kumekuwa na shaka kwa muda mrefu katika mkoa wa pwani nchini Kenya kwamba vuguvugu la Mombasa Republican Council- MRC, litazima jaribio lolote la serikali kuandaa uchaguzi mkuu katika mkoa huo, wakisema pwani sio sehemu ya Kenya.

Mwandishi wa VOA mjini Mombasa anaripoti kuwa hapo awali, kulikuwa na kesi katika mahakama kuu ya Kenya ikitaka tume ya uchaguzi na mipaka, isitishe zoezi hilo, lakini kesi hiyo haikufaulu kortini.

Kinyume kabisa na msimamo huo, wakati Wakenya wakishiriki kura ya Mchujo kuanzia Alhamisi asubuhi kujiandaa kwa uchaguzi mkuu, viongozi wa MRC wameamua kuhubiri amani, na kupinga tetesi kuwa watazuia uchaguzi.

Msemaji wa kundi hilo Rashid Mraja ameondoa MRC lawamani, kuhusu madai kwamba wanachama wake wamekuwa wakizuru jimbo la Tana River, na kuhusika na mauaji katika wilaya ya Tana Delta.

Hali ya Usalama katika mikoa tofauti ni Kigezo muhimu kinachofuatiliwa kwa makini huko Kenya hata waangalizi wa kimataifa, kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 4 mwezi Machi mwaka huu.
XS
SM
MD
LG