Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 13:43

Wanamgambo wa kiislam wenye uhusiano na Alqaeda wanashikilia watu 41.


Waziri wa Ulinzi Leon Panetta akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Wanamgambo wa kiislam nchini Algeria wenye uhusiano na Al qaida wanawashikilia watu wapatao 41 ambao walikuwa wakifanya kazi katika eneo la gesi ya asili kwa kile wanamgambo wanakiita ni kulipiza kisasi kwa hatua za jeshi la ufaransa nchini Mali.
Msemaji wa alqaeda katika eneo la Afrika magharibi (AQIM) aliiambia Sauti ya Amerika kwamba wamarekani saba walikuwa ni kati ya waliotekwa nyara. Wengine wanafikiriwa kuwa ni pamoja na Waingereza , Wafaransa na WaNorway.
Msemaji Oumar Ould Hamaha alisema Jumatano kama wamarekani wanataka kusaidia Ufaransa watakumbana na matatizo.
Anasema Ufaransa imetangaza vita na watu wa magharibi wataumia kama vita hivyo vikiendelea.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Pannetta amesema ukamataji huo ni kitendo cha kigaidi. Anasema Marekani itachukua hatua zote madhubuti kuweza kupambana na hali hiyo.
XS
SM
MD
LG