Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:45

Marekani yamtaka Rais wa Misri kufuta usemi wake.


Rais Barack Obama
Rais Barack Obama
Marekani imemtaka rais wa Misri Mohamed Morsi kufuta usemi wake wa maneno ya kichochezi dhidi Waisrael aliyotoa kabla ya kuchaguliwa.

Kwa mujibu wa kipande cha habari kilichotolewa kwenye televisheni wiki iliyopita na Middle East Media Research Institute, mwaka 2010 bwana.Morsi aliwaelezea Waisraeli kama wavamizi wa Palestina na pia kama wanyonya damu na wapenda vita na kizazi cha nguruwe na nyani.

Alitoa maneno mengine yasiyo ya kweli na kuwataka raia wa Misri kuwafundisha watoto wao kuchukia wayahudi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Viktoria Nuland aliwaambia waandishi wa habari jumanne kwamba Washington inalaani maneno yaliotolewa na rais Morsi.
XS
SM
MD
LG