Majeshi ya Mali yalipambana na wapiganaji wa kiislam wakati wanamgambo wakijaribu kwa mara ya pili wiki hii kuingia ndani zaidi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Mali.
Afisa wa juu wa jeshi la Mali akiongea kwa kwa misingi ya kutotajwa jina ameiambia VOA kwamba mapigano hayo yalitokea katika mji wa Kona, ambao upo karibu na eneo linalodhibitiwa na serikali kati kati ya nchi.
Mwandishi wa VOA katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo karibu na mapigano alisema malori yaliojaa wapiganaji wa kiislam yaliondoka kuelekea uwanja wa mapambano baada ya ghasia kuripotiwa kumalizika jumatano usiku .
Msemaji wa Ansar Dine moja ya makundi yanayopambana na serikali alikataa kuielezea VOA juu ya mipango yao kama wataingia zaidi upande wa kusini.
Mpaka sasa jeshi limeweka wanamgambo wa kiislam nje kidogo ya Mopti, eneo lililo ngome ya serikali. Majeshi ya Mali yalipambana na wanamgambo katika eneo hilo wiki hii.