Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:55

Wafuasi na wapinzani wa Rais Morsi wapambana Cairo.


Rais wa Misri Mohammed Morsi.
Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri Mohamed Morsi walipambana Jumanne usiku huko Cairo kwa mawe na mabomu, wakati washauri wakuu watatu wa rais huyo wakijiuzulu kupinga jinsi anavyoendesha mzozo wa kikatiba wa nchi hiyo.

Akiripoti kutoka Cairo mwandishi wa VOA Elizabeth Arrot amesema ghasia hizo mpya ziliibuka wakati wafuasi wa kiislam wa Morsi waliposhambulia waandamanaji wakipinga kile walichokiita unyakuzi wa madaraka wa rais Morsi.

Arrott anasema wafuasi wengi wa rais walikuwa wanaume wenye madevu wakionekana kuwa moja kwa moja ni wafuasi wa Muslim Brotherhood ambao walishambulia waandishi wa habari nje ya jumba la rais.

Wakati huo huo washauri wengine watatu wa rais walitangaza kujiuzulu wakipinga amri ya rais kujipa madaraka zaidi .Watano kati ya washauri wa rais 17 wamejiuzulu tangu Novemba 22.
XS
SM
MD
LG