Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:25

Waasi wa M23 waondoka kwenye miji waliyoteka DRC.


Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.
Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.
Wakazi wa mji wa Sake ashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wanasema wanajeshi waasi wa kundi la M23 wamevamia nyumba na kuiba pesa kutoka kwa wafanyabiashara wakati wanajiandaa kuondoka katika eneo hilo.

Pembeni mwa barabara kwenye mji wa Sake nje ya eneo ambalo kundi la M23 linalinda kituo cha ukaguzi, kundi na wakazi wanalalamika kuhusu magenge ya waasi waliouvamia mji wakati wa usiku.

Mkazi mmoja aliyekataa kusema jina lake alionesha madirisha mawili yaliyoharibiwa katika nyumba yake ambayo anasema wanajeshi walivunja kwa kutumia bunduki zao wakati familia yake ikila chakula cha jioni.

Anasema waliingia ndani ya nyumba hiyo saa saba usiku . Walichukua pesa magodoro na kila kitu, walipoamka asubuhi hawakukuta kitu.

Katika makutano makuu ya barabara mjini humo, madereva wa magari makubwa wamesimama pembeni mwa magari yao. Wanasema waasi wamewataka walipe dola 320 ili waweze kuondoka mjini na hawawezi kwenda popote mpaka wapate pesa.

Waasi walichukua udhibiti wa mji wiki iliyopita baada ya mapigano makali na jeshi la congo.

Lakini sasa kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na kundi la M23 na jeshi la Congo waasi wanajiandaa kuondoka kwenye mji wa Sake na mji ulio karibu wa Goma.
XS
SM
MD
LG