Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:05

Rais wa Nigeria apongeza ushindi wa Gavana kutoka upinzani.


Rais wa nigeria katikati, Goodluck Jonathan.
Rais wa nigeria katikati, Goodluck Jonathan.

Baada ya kupoteza kinyang’anyiro cha kiti cha ugavana katika jimbo la Southern Ondo , chama tawala cha Nigeria kimegawanyika. Viongozi wa chama tawala cha Ondo wametoa wito kufanyika uchunguzi wa tuhuma za wizi wa kura wakati rais Goodluck Jonathan akisema kuwa uchaguzi ni ishara ya utamaduni wa kidemokrasia.

Katika uchaguzi wowote wa ndani nchini Nigeria siku hizi mahangaiko ni yaleyale katika kinyang’anyiro cha kutafuta uungwaji mkono kwenye uchaguzi wa urais wa mwaka 2015.

Upande wa kusini ambako anatoka rais Goodluck Jonathan umeonekana kupata upinzani mkubwa .Ni eneo ambalo pia hawezi kuwa tayari kulipoteza Kama atagombea tena.

Ovie joseph ni mwanachama wa chama tawala cha people’s demokratid party na afisa wa zamani wa chama. Katika makazi yake ya jimbo la delta, anasema watu wa kusini wanapoteza hamu yao kwa arais hali iliyopelekea kushindwa katika uchaguzi wa Ugavana.

Gavana aliyoko madarakani Olusegun Mimiko mwanachama wa Labor Party kundi dogo lenye kujulikana kwa kadri katika eneo kubwa la nchi alishinda katika uchaguzi wa ugavana uliofanyika mwishoni hivi karibuni kwa asilimia 46 ya kura. Hii inakuja baada ya uchaguzi wa julai kwenye jimbo la Edo , pia kusini ambalo lilichukuliwa na chama kikuu cha upinzani , The Action Congress of Nigeria.

Jumanne gavana mimiko alikubali rasmi kuingia madarakani na kumpongeza rais kwa kile alichosema kilikuwa ni uchaguzi wa amani na haki.

Tangu kufanyika uchaguzi chama tawala kiligawanyika katika uchaguzi. Katika mji mkuu rais Goodluck Jonathan alitoa taarifa za pongezi kwa gavana na kuahidi uungwaji mkono wake.
XS
SM
MD
LG