Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 23:56

Octoba saba : Maadhimisho ya vita vya Afghanistan


Mwanajeshi wa Marekani akipiga doria kwenye kituo cha polisi baada ya shambulio la wanaharakati. June 19, 2012.
Mwanajeshi wa Marekani akipiga doria kwenye kituo cha polisi baada ya shambulio la wanaharakati. June 19, 2012.

Octoba saba ni maadhimisho ya miaka 11 ya kuanza vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.

Vimedumu kwa muda mrefu zaidi kuliko vita vingine katika historia ya Marekani. Zaidi ya wanajeshi 3000 wa kimataifa wamekufa katika vita ikiwemo wamarekani 2000.

Raia wa Afghanistan pia wamekufa katika vita hivi. Vita vilichochewa na mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani Septemba 11 mwaka 2001 .

Chini ya mwezi mmoja baadae vikosi vya jeshi la Marekani viliingia katika ardhi ya Afghanistan kushambulia kundi la wanamgambo wa Al- qaida na serikali ya utawala wa Taliban ambayo iliongoza mtandao wa kigaidi. Taliban iliondolewa haraka.

Lakini wanamgambo waasi wameongeza nguvu kwa miaka kadhaa. Marekani na vikosi vya kimataifa vya pamoja vimekabiliwa na mfululizo wa mashambulizi yanayojulikana kama “mashambulizi ya ndani” yanayofanywa dhidi ya jeshi la muungano wa nchi za magharibi na wanajeshi na polisi wa Afghanistan.

Majeshi ya pamoja yameanza kujiondoa nchini humo huku majeshi yote ya kigeni wamepanga kkuondoka ifikapo mwaka 2014.
XS
SM
MD
LG