Upatikanaji viungo

Mkuu wa bandari ya Dar Es Salaam asimamishwa kazi


Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Dkt Harisson Mwakyembe, akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam
Wazirir wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari - TPA Bw. Ephrahim Mgawe pamoja na manaibu wake wawili ili kuruhusu uchunguzi ufanyike kutokana na malalamiko ya uzembe wa kazi.

Maafisa wengine walosimamishwa kazi ni meneja wa mafuta ya ndege, meneja wa Jet na yule wa kituo cha mafuta, kutokana na tuhuma za za kupotea mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta safi na machafu.

Akizungumza na sauti ya Amerika Waziri Mwakyembe anasema alilazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na malalamiko kadhaa aliyopokea kuanzia kupotea kontaina bandarini, kuchelewa kuondolewa bidhaa, hadi kupotea mafuta.Bw. Mwakyembe anasema ameteuwa tume maalum kufanya uchunguzi na kumwasilishia ripoti katika muda wa siku 14 kabla ya kuweza kuchukua uwamuzi wa kuendelea mbele na kuhakikisha bandari ya Dar es salaama inafanya kazi kwa uzuri na ustadi kabisa.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG