Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:09

Wanaharakati wa Mali wakata mkono wa mwizi


Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.
Wanajeshi wanaotawala Mali wakiwa wanalinda makao makuu yao.
Wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali kaskazini mwa Mali wameukata mkono wa mtuhumiwa mwizi kama sehemu ya juhudi za kusimika sheria kali za kiislamu.

Mashahidi wanasema kundi kubwa la watu lilishuhudia kukatwa kwa mkono wa mtu huyu Jumatano katika kijiji cha mbali cha Ansongo. Wanachama wa kundi la Movement for Oneness and Jihad Afrika Magharibi wanasema adhabu hiyo ilitolewa kufuata misingi ya Sharia za Koran.

Mtu huyo alituhumiwa kuiba baiskeli. Hili ni tukio la kwanza kutangazwa la utekelezaji wa Sharia ya Kislamu kaskazini mwa Mali tangu makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali kuchukua udhibiti wa eneo hilo mwezi juni.

Jumapili waandamanaji walizuia wanamgambo kukata mkono wa mwizi katika mji wa Gao.
XS
SM
MD
LG