Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:34

Clinton akutana na Mandela kijijini Qunu


Hillary Clinton akutana na Nelson Mandela na Mkewe Graca Machel (k) nyumbani kwake Qunu, Afrika Kusini
Hillary Clinton akutana na Nelson Mandela na Mkewe Graca Machel (k) nyumbani kwake Qunu, Afrika Kusini
Waziri wa mambo ya nje wa marekani Hillary Clinton yupo nchini Afrika kusini ambapo amekutana kwa faragha na kiongozi aliyeongoza upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela.

Clinton alisafiri kuelekea kwenye kijiji cha Qunu jumatatu kukutana na Rais huyo wa zamani nchini humo. Bwana mandela mwenye umri wa miaka 94 afya yake imezorota na haonekani hadharani kama ilivyokuwa awali.

Clinton kisha alikwenda Johannesburg kuhudhuria mkutano wa maafisa wa vyeo vya juu kati ya Marekani na Afrika kusini pamoja na wakurugenzi wa biashara.
Clinton amekuwa akihamasisha uwekezaji na biashara kwa Marekani wakati wa ziara yake ya siku 10 barani Afrika.

Afrika kusini ni soko kuu la bidhaa za Marekani wakati Marekani ni mpelekaji mkuu na muwekezaji katika soko la Afrika kusini.

Afrika ni eneo lenye baadhi ya nchi zinazokua kiuchumi haraka sana na idadi ya watu duniani. Kuongeza uchumi na uwekezaji katika bara hilo imekuwa ni sehemu muhimu ya sera za nje za Marekani.

Marekani ni rafiki mkubwa wa Afrika katika biashara baada ya China. Baada ya ziara ya waziri Clinton nchini Afrika kusini anatarajiwa kusafiri kuelekea Nigeria, Benin na Ghana.
Nchi alizotembelea awali katika ziara hiyo ilikuwa Kenya, Uganda, Sudan Kusini na Senegal.
XS
SM
MD
LG