Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 14:58

Assad:Mapambano na waasi kuamua hatima ya nchi


Moshi unapaa baada ya majeshi ya Syria kufyetua mizinga kwenye vitongoji vya Damuscus

Rais wa Syria Bashar Al Assad amesema jeshi la nchi yake liko kwenye mapambano na waasi yatakayoamua hatima ya nchi hiyo. Bw.Assad alisifu majeshi ya serikali katika taarifa yake ya Jumatano wakati ghasia zikiendelea kote nchini Syria.

Mapambano makali yaibuka kwa mara ya kwanza katika eneo lenye wakristo wengi Damascus.Shirika lenye makao yake Uingereza Observatory for human Rights lilisema mtu mmoja aliuwawa katika mapigano kati ya majeshi ya Syria na upinzani katika eneo lenye wakristo wengi huko Damascus.

Hakujawa na mapigano mengi katika maeneo yenye wakristo wengi nchini humo tangu uasi dhidi ya utawala wa rais Assad kuanza miezi 17 iliyopita.

XS
SM
MD
LG