Sudan imekuwa kitovu cha vita kwa muda wa mwaka mmoja sasa, ambayo imetokana na kuhasimiana kati ya jeshi na vikosi vya akiba vya RSF.
Wanakikosi maalumu cha jeshi maalumu la Kimapinduzi la Iran, walishuka kutoka kwenye helikopta kuingia katika meli ya makasha yenye uhusiano na Israel, karibu na mlango wa bahari wa Hormuz na kuikamata meli hiyo Jumamosi.
Wakati tukiendelea kufutilia mambo kwenye michuano ya Afcon, huko Ivory Coast, wapenzi wa kandanda Jumatano wanasubiri kwa hamu kuona namna mambo yatakavyokuwa kati ya Morocco na Tanzania kwenye uwanja wa San Pedro.
Kundi la watu takribani 250 kutoka jamii ya walio wachache walioteswa huko Myanmar waliwasili katika jimbo la Aceh siku ya Alhamisi, lakini wakaazi waliwaambia wasiingie katika eneo hilo.
Watafiti wamesema kwamba wilaya zilizo katikati mwa Sydney zinakaribia kuwa sehemu za kwanza duniani kufikia lengo la Umoja wa Mataifa, la kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya Ukimwi – HIV.
Shirika la afya duniani WHO, na washirika wake wamesema kwamba karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani, zitatolewa kwa nchi 12 za Afrika ifikapo mwaka 2025.
Siku ya Wakimbizi duniani, ambayo huadhimishwa Juni 20, mwaka huu siku hii inasherehekea ujasiri, uvumilivu, na ushujaa wa mamilioni ya watu ambao wanazikimbia nchi zao ili kuepuka migogoro au mateso.
Rosa Yusif Elias alitoroka Sudan kwa miguu akiwa na watoto wake saba kupitia mpakani kwenda kwenye nchi yake ya Sudan Kusini kwa ajili ya kutafuta usalama.
Kenya itaubadilisha msitu mkubwa wa Shakahola ulioko pwani ya nchi hiyo kuwa kumbukumbu la kitaifa, eneo hilo ambalo miili ya watu zaidi ya 250 ilifukuliwa na kuhusishwa kuwa ni ya wafuasi wa ibada ya siku ya kiyama, waziri mmoja amesema.
Wanaharakati wa kutetea maziringa katika nchi za Afrika mashariki na kati wanayataka makampuni ya kutengeneza vifaa vya kielectroniki na bidhaa za plastiki kuweka utaratibu na kulipia gharama za ukusanyaji na uchakataji wa bidhaa hizo ili kulinda mazingira, viumbe hai na afya za binaadamu.
Mahakama ya Kenya siku ya Ijumaa iliamuru kusimamisha kufukuza kazi kwa wasimamizi wa maudhui kadhaa walioajiriwa na kampuni mkandarasi ya Sama inayofanya kazi na Meta, kampuni mama ya Facebook.
Wakulima wa tumbaku wa mkoa wa Tabora, nchini Tanzania wamesema serikali imeshindwa kutekeleza hatua za kuliondoa zao hilo, na kuwahamashisha wakulima kuingia kweney kilimo cha mazao ya chakula ambayo yataweza kuwaingizia kipato.
Pandisha zaidi