Alhamisi, Aprili 24, 2014 Local time: 00:42

Habari / Afrika

Wamisri wapigia katiba kura

Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.      Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.
x
Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.
Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.
ukubwa wa habari - +
Nusu ya wapiga kura waliosajiliwa nchini Misri wamepiga kura leo Jumamosi  juu ya rasimu yenye utata ya katiba, ambayo imezusha vurugu na maandamano kwa wiki kadha  sasa nchini humo.

Wanaume na wanawake walipigia kura zao katika shule tofauti  mjini Cairo na mikoa mingine 9.Rais wa Misri Mohammed Morsi  pia alipiga kura yake  Jumamosi. Wapiga kura wengine watapigia rasimu hiyo kura Jumamosi ijayo Desemba 22.

Kura hiyo imepangiwa kufanyika  Jumamosi  moja baada ya nyingine kutokana na wito wa kuisusia  uliotolewa na wengi katika mfumo wa mahakama  nchini humo ambao sharti wasimamie kura hiyo kwa mujibu wa sheria za Misri.

Haijabainika matokeo ya mwisho yatatangazwa lini. Chama cha zamani cha rais Morsi Muslim Brotherhood kinaunga mkono katiba iliyopendekezwa. Morsi alijiuzulu kutoka chama hicho baada ya kuwa rais mapema mwaka huu. Makundi  ya upinzani  wenye msimamo wa kadri, pamoja na Wakristo wana hofu kuwa katiba inayopendekezwa itahujumu haki zao na kuzipa nguvu zaidi sheria  kali za kiislam sharia na haisemi chochote kuhusu haki za wanawake.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mafuriko Dar-es Salaam - VOA MItaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
16.04.2014 14:06
Karibu watu 10 wamefariki na maelfu kuharibiwa makazi yao jijini Dar es Salaam kufuatia mvua kali ya siku chache.