Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 07:10

Wakenya washinda mbio za Marathon za London


Wilson Kipsang, wa Kenya akimaliza kama mshinda wa mbio za Marathon za London 2014
Wilson Kipsang, wa Kenya akimaliza kama mshinda wa mbio za Marathon za London 2014
Kijiji cha Iten nchini Kenya kilijitangazia kuwa “makazi bingwa wa mbio za masafa marefu” kufuatia mazingira yaliyojionesha Jumapili kijijini hapo kwenye mji mkuu wa kaunti ya Elgeyo Maraket kufuatia ushindi wa pili wa Wilson Kiprotich Kipsang kwenye mbio ndefu zijulikanazo London Marathon zilizofanyika jijini London , Uingereza.

Kipsang alivunja rekodi kwenye mbio za “London Marathon” kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili, dakika nne na sekunde 27.

Aliibuka mshindi dakika chache baada ya jirani yake kutoka kijiji hicho hicho cha Iten na mshindi wa mara mbili duniani, Ednah Ngeringwony Kiplagat alishinda mbio za wanawake kwa kutumia saa mbili dakika 20 na sekunde 21 huku akimshinda mwanamke mwingine mkazi wa kijiji cha Iten, Florence Kiplagat.

Kipsang na Kiplagat wanaishi umbali wa mita 700 kutoka kila moja katika eneo la Mindililwa katika kijiji cha Iten na wote walipigiwa kura ya kuwa wanariadha bora zaidi kwa mwaka 2013 na taasisi kubwa duniani inayohusika na masuala ya wanariadha AIMS.

Wakati huo huo mke wa Rais Uhuru Kenyatta, bibi Margaret Kenyatta alikimbia katika mbio za London Marathon kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya taasisi yake inayoitwa “Beyond Zero” ya kusaidia wananchi wa Kenya kupata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi, ambayo inahamasisha watu kuchanga fedha za kuweka zahanati 47 za muda kwa ajili ya kutoa huduma za afya.

Umati ulikuwa unaanza kuondoka kwenye uwanja wa riadha mwendo wa saa 12 jioni kwa saa za London wakati habari ziliposambaa kote London kwamba mke wa Rais Kenyatta amevuka kilomita 32 katika mbio za kilomita 42.195 akiwa miongoni mwa mashabiki 36,000 na wanariadha wafadhili waliojitolea kusaidia taasisi yake kwa ajili ya watu maskini.
XS
SM
MD
LG