Jumatatu, Mei 25, 2015 Local time: 06:11

Habari / Afrika

Mawaziri wa Afrika na Ulaya wajadili usalama Mali

Waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Hubert Coulibaly akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Waziri wa mambo ya nje wa Mali Tieman Hubert Coulibaly akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari.
Wakati vikosi vya Chad vinasaidia kudhibiti mji muhimu ulioko  jangwani, huko Mali, wawakilishi wa mataifa ya Kiafrika na ya Ulaya walikutana mjini Brussels Jumanne kujadili uwezekano wa kubuni kikosi cha kimataifa kusaidia kudhibiti taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wawakilishi hao walisema uamuzi wowote wa kugeuza kikosi cha nchi za Afrika magharibi kuwa kikosi cha kimataifa cha kuleta uthabiti nchini Mali, lazima kipitishwe na Umoja Mataifa na serikali ya Mali.

Desire Ouedraogo, ambaye anaongoza tume ya jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS, alisema matatizo ya Mali sio suala tu la usalama wa kitaifa au wa kikanda, lakini ni suala la usalama wa kimataifa. Alisema jumuiya ya kimataifa lazima ihakikishe kuwa Mali kaskazini haitumiwi  kuwa hifadhi ya magaidi na walanguzi wa madawa haramu.

Matamshi yake yalifuatia mazungumzo miongoni mwa wawakilishi wa mataifa ya jumuiya ya  Ulaya, Afrika na Umoja Mataifa, juu ya jinsi ya kuratibu juhudi  za kuleta uthabiti huko Mali, baada ya wanamgambo wa kiislamu kuzusha  mzozo wa kisiasa. Serikali ya Mali imeahidi kufuata masharti ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa ulaya Catherine Ashton, alisema ulaya tayari inatimiza ahadi yake ya kusaidia kulipatia mafunzo jeshi la Mali, na imetenga zaidi ya dola millioni mia 4 za msaada kwa mwaka huu kusaidia taifa hilo la Afrika magharibi.

Hadi sasa, Ufaransa imekuwa nchi pekee ya Ulaya kupeleka wanajeshi huko Mali. Mashambulizi ya vikosi vya Ufaransa yaliyofanikiwa  kuwarudisha nyuma wanamgambo wa kiislamu, yamepongezwa sio tu kutoka kwa waafrika, lakini viongozi wa nchi za magharibi kadhalika, ikiwa ni pamoja na makam rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alikutana na rais wa Ufaransa Francois Hollande Jumatatu huko mjini Paris.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.