Alhamisi, Mei 28, 2015 Local time: 04:47

Habari / Afrika

Barabara yapatiwa jina la Rais Kibaki mjini Dar es Salaam

Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais wa Kenya Mwai Kibaki  amefanya ziara nchini Tanzania ambayo ametumia kama njia ya kutoa mkono wa kwaheri wakati huu ambapo kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu machi 4 mwaka huu.

Ripoti ya Dina Chahali
Ripoti ya Dina Chahali, Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Moja ya kumbukumbu kubwa aliyopata katika ziara yake ya kuwaaga watanzania waliopo jijini Dar Es Salaam ni kupewa jina lake katika moja ya barabara maarufu iliyokuwa ikijulikana kama Old Bagamoyo Road  na sasa inaitwa “MWAI KIBAKI ROAD".
 
Rais Kibaki akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete alizindua barabara hiyo Alhamis yenye jina  la barabara ya Mwai Kibaki.

Barabara hii kwa mujibu wa meya wa manispaa ya Kinondoni Rajab Mwenda ina historia ya kuwa imepita katika makazi ya marais wote wa Tanzania tangu muasisi wa taifa la Tanzania  hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais wa sasa Jakaya Kikwete.

Shughuli nyingine iliyofanyika katika ziara ya Rais Kibaki nchini Tanzania ni mazungumzo aliyoyafanya Rasi huyo wa Kenya na wazee wa mkoa wa Dar Es Salaam ambapo Rais Kibaki alisisitiza kuimarisha ushirikianao wa kibiashara baina  ya nchi hizi mbili ili kuchochea kasi ya maendeleo katika ukanda huu  wa Afrika mashariki.

Kenya na Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umeimarishwa zaidi hivi  sasa katika mtengamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.