Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:53

Polisi Kenya waepusha shambulizi la kigaidi


Vikosi vya usalama Kenya katika doria
Vikosi vya usalama Kenya katika doria

Polisi wanasema wametia nguvuni fulana zinazovaliwa na wajitoa mhanga, bunduki, risasi na mabomu ambayo inaelekea vilikuwa vinatayarishwa kutumiwa katika shambulizi la kigaidi

Polisi wa Kenya wanasema wameepusha shambulizi kubwa la kigaidi likiwa katika hatua za mwisho za matayarisho, na kukamata watu wawili wakiwa na milipuko, silaha na risasi.

Watu hao wawili walikamatwa katika mtaa wenye wahamiaji wengi wa Kisomali mjini Nairobi, alisema Boniface Mwaniki, mkuu wa kikosi cha kupambana na ugaidi. Alisema watu hao wanashukiwa kuwa na uhusiano na makundi ya al-Shabab la Somali linalosemekana kuwa na uhusiano na al-Qaida.

Polisi walikuta fulana nne za kujitoa mhanga, mabomu mawili, bunduki nne aina ya AK-47, risasi na mabomu 12 ya mkononi, alisema na kuongeza kuwa fulana hizo ni sawa na zile zilizotumiwa katika shambulizi la Uganda katika kundi la watu waliokuwa wakiangalia mpira mwaka 2010 na kuuwa watu 76.
XS
SM
MD
LG