Jumapili, Mei 24, 2015 Local time: 05:46

Habari / Afrika

Hotuba ya rais Obama juu ya hali ya kitaifa

Rais Obama aliwarai wabunge wa vyama vyote viwili kundoa tofauti zao za kisiasa katika maswala makuu ya kuimarisha Marekani.

Rais Barack Obama, akitoa hotuba ya hali ya kitaifa Feb. 12, 2013
Rais Barack Obama, akitoa hotuba ya hali ya kitaifa Feb. 12, 2013
                
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake Jumanne usiku juu ya hali ya kitaifa. Mojawapo ya maswala aliyoyapa uzito yakiwa swala la uchumi na ajira. Akigusia moja ya mambo yenye utata  Bw. Obama alitoa wito tena kuwe na juhudi madhubuti za kufanya mabadiliko katika sheria juu ya umilikaji wa silaha.

Alisema  yale machache  aliyozungumzia  katika hotuba ya Jumanne usiku  yatakuwa muhimu ikiwa mabaraza ya bunge yatakubaliana kulinda kile alichosema ni raslimali muhimu sana -nao ni watoto. Pia aliwataka wabunge kupigia kura mswada wa kuchunguza  historian na tabia za  watu wanaonunua bunduki na kuondoa silaha za kijeshi mitaani ili kulinda maisha ya raia wa Marekani wanaoendelea kuuawa kiholela na watu wenye bunduki .

Ghasia za bunduki zimekuwa suala kubwa tangu mauaji ya halaiki ya mwezi Desemba ya katika shule ya watoto ya Sandyhook jimbo la Connecticut .

Rais Obama aliahidi tena kuhakikisha nafasi sawa kwa wanajeshi wote ikiwa ni pamoja na mafao kwa familia zao hata kwa wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Amesema pia wanajeshi wa Marekani wataondoka Afghanistan kama ilivyopangwa mwaka wa 2014 na kwamba Marekani  ni taifa lenye  bora zaidi kuliko yote duniani.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.