Jumanne, Septemba 23, 2014 Local time: 10:18

Habari / Marekani

Dunia yaukaribisha mwaka 2013

Fataki zikirushwa huko Sydney, Australia kusheherekea mwaka mpya.
Fataki zikirushwa huko Sydney, Australia kusheherekea mwaka mpya.
Fataki nyingi zimerushwa kwenye bandari ya  Sydney, Australia na mataifa mengine ya Pacific yamekuwa ya kwanza kuukaribisha mwaka mpya wa 2013 .

Kiasi cha watu milioni 1.5 walizunguka bandari ya Sydney na kuona maonyesho  ya fataki zilizo gharimu dola  milioni 6.9  huku wengine wakipiga kambi nje kwa karibu siku nzima ili kupata nafasi ya kujionea sherehe hizo vizuri. Watu wengi zaidi walifuatilia matukio haya kwenye televisheni duniani kote wakati nyota wa muziki wa Australia, Kylie Minogue alipobonyeza kitufe cha kuanza sherehe za mwaka mpya huku  wimbo wake ukipigwa na watu wakichezwa.

Huko Japan mamilioni ya watu walikuwa wakitembelea nyumba ya sala ya Shinto na hekalu la wabudha kwa sherehe za mwisho za kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha  mwaka 2013.  Na nchini Marekani tungali saa chache nyuma watu wakisubiri pia kuukaribisha mwaka mpya kwa kujumuika pamoja kwenye sherehe mbalimbali.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.