Jumatano, Julai 23, 2014 Local time: 22:01

Habari / Dunia

Baba wa msichana wa kihindi aliyebakwa atoa ruhusa ya kutaja jina la mwanae.

Mwanafunzi akisali wakati wa ibada ya muathirika wa kubakwa India.Mwanafunzi akisali wakati wa ibada ya muathirika wa kubakwa India.
x
Mwanafunzi akisali wakati wa ibada ya muathirika wa kubakwa India.
Mwanafunzi akisali wakati wa ibada ya muathirika wa kubakwa India.
Baba wa msichana wa kihindi aliyebakwa na watu wengi na baadaye kufariki dunia kutokana na kuumia vibaya amesema anataka kutoa ruhusa ya kutaja jina la mtoto wake ili kuwapa nguvu watu wengine walioathiriwa na ghasia za ngono.
 
Baba huyo aliliambia jarida la kila Jumapili la People la Uingereza    kwamba mtoto wake hakufanya chochote kibaya na alikufa wakati akijilinda.
 
Amesema ana fahari kubwa na mwanae na kutaja jina lake anatumai kutawapa matumaini wasichana wengine ambao wamekutana na matatizo kama hayo.
 
Pamoja na maandamano kadhaa nchini India dhidi ya ukatili huo mbaya  kumekuwa na wito wa kitaifa kumtaja msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23  ikiwa ni pamoja na pendekezo la kutangaza sheria mpya yenye jina lake ya kupambana na ubakaji .

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maoni ya Wakenya kuhusu Sabasabai
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
04.07.2014 15:03
Baadhi ya Wakenya waeleza maoni yao kuhusu mkutano wa hadhara ulioitishwa na wanasiasa wa Cord katika uwanja wa Uhuru Park mjini Nairobi