Jumapili, Novemba 23, 2014 Local time: 10:06

Habari / Afrika

Waasi wa Congo wakubali kuondoka Goma

Kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Brigadia-General Sultani Makenga huko Goma, Kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Brigadia-General Sultani Makenga huko Goma,
x
Kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Brigadia-General Sultani Makenga huko Goma,
Kiongozi wa kijeshi wa kundi la M23 Brigadia-General Sultani Makenga huko Goma,
Mkuu wa kisiasa wa kundi la M23  amesema majeshi yake yataondoka  katika mji  wa  Goma mara moja kama serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo  itatekeleza  madai yao.

Jean Marie Runinga aliongea na waandishi wa habari Jumanne huko Goma  mji ambao ulichukuliwa na waasi  wiki iliyopita na baada ya hapo  kuchukua mji wa  Sake upande wa magharibi.

Mapema  Jumanne , mkurugenzi wa mahusiano  ya nje wa M23 Rene Abandi aliiambia VOA kwamba mkuu wa jeshi wa kundi hilo aliahidi  majeshi yake yataondoka Goma haraka iwezekanavyo, baada ya mkutano na wakuu wa jeshi wa Uganda , Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. 

Abandi alisema hatua hiyo haifanywi kwa shinikizo, ila ilikuwa ni dalili ya  waasi kuridhia  kufanya mazungumzo na serikali.

Wakati huo huo maafisa wa jeshi la Rwanda wanasema wahutu wenye msimamo mkali waliopo  mashariki mwa Congo waliingia Rwanda Jumanne na kushambulia vijiji karibu na mpaka.

Msemaji wa jeshi alilaani majeshi ya waasi wa Rwanda (FDLR) kwa shambulizi hilo ambalo limepelekea mapigano na jeshi la Rwanda.

Shirika la habari la Reuters linaripoti Rwanda FDLR  inayoipinga  serikali  ya Rwanda inayoongozwa na watusi imekataa kuwa inahusika na mapigano yeyote.

Rwanda imesema washambuliaji hao wanaofikia 100, walirudishwa nyuma na kurejea  DRC au kwingineko nchini Rwanda . Imesema wapiganaji 6 wa FDLR waliuwawa na wawili kukamatwa na raia mmoja aliuwawa
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  60 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Usafiri wa Bodaboda Dar es Salaam - Voamitaanii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.11.2014 08:18
Wasfiri wa Bodaboda waeleza maadhui yao na usafiri huo katika jiji la Dar Es Salaam.