Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:50

Al-Shabaab washambulia kituo cha AMISOM Mogadishu


Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab lenye makao yake huko Somalia
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab lenye makao yake huko Somalia

Maafisa na mashuhuda walisema wanamgambo wa kundi la al-Shabaab la nchini Somalia wameshambulia kituo cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji wa Leego huko kusini mwa Somalia.

Wanamgambo walikuwemo kwenye gari lililojaa milipuko na kuingia kwenye mlango mkuu wa kituo hicho kisha kufuatiwa na mapigano makali ya bunduki na wanajeshi wa Burundi ambao wanalinda kituo hicho.

Vyanzo vinasema wanamgambo waliingia kwenye kituo na kuchukua udhibiti wa sehemu ya kituo hicho. Mji wa Leego ni kiasi cha kilomita 130 kusini ya Mogadishu na ni moja ya barabara kuu inayounganisha Mogadishu na Baidoa.

AMISOM ilithibitisha kwamba kulikuwepo na shambulizi linaloendelea kwenye kituo chao ambalo lilianza mapema asubuhi ya Ijumaa.

Vyanzo vili-ithibitishia Sauti ya Amerika-VOA kwamba Zaidi ya wanajeshi 50 wa Burundi wanakhofiwa kuuwawa katika shambulizi hilo. Gavana wa jimbo la Lower Shabelle, Abdikadir Mohamed Nur Siidi alithibitisha kwamba kuna idadi kadhaa ya vifo kwa upande wa wanajeshi wa umoja wa Afrika.

Gavana huyo alisema darzeni ya wapiganaji wa kundi la al-Shabaab waliuwawa wakiwemo wajitoa mhanga 15 ambao walijilipua wenyewe. Pia alisema wanamgambo waliwateka darzeni ya watu akiwemo naibu wa wilaya ya kijiji cha Leego, Abukar Abdilaahi Geedi ambaye ni miongoni mwa watu waliopotea.

Wanamgambo wa kundi la al-Shabab
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab

Msemaji wa kundi la al-Shabaab alidai kwamba kundi hilo liliuwa Zaidi ya wanajeshi 50 wa Burundi. Hili ni shambulizi la karibuni kati ya mashambulizi kadhaa yaliyoripotiwa ya al-Shabaab tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan wiki iliyopita.

Wanajeshi wa Somalia na AMISOM walifanikiwa kuwavurumusha wanamgambo wa kundi la al-Shabaab kutoka miji mikubwa ya Somalia lakini kundi hilo bado linadhibiti maeneo mengine na linaendelea kufanya mashambulizi.

XS
SM
MD
LG