Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:57

Afrika ya Kati yazungumzia mgogoro wa CAR


Watu wakiwa chini ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati, Francois Bozize mjini Bangui, December 28, 2012
Watu wakiwa chini ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati, Francois Bozize mjini Bangui, December 28, 2012
Mataifa ya Afrika ya kati yanashughulikia mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kundi la uasi la Seleka ambalo limechukua udhibiti wa miji 10 katika upande wa kaskazini katika kipindi cha zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Huku waasi hivi sasa wakiwa wanadhibiti eneo la kiasi cha kilomita 300 kutoka mji mkuu Bangui, kilichobaki kulinda amani ni wanajeshi wapatao 100 tu kutoka nchi jirani ya Chad na jeshi la kieneo kutoka nchi za jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi -ECOWAS ambazo zimeahidi kupeleka wanajeshi huko.

Alhamis Rais Francois Bozize aliitaka Ufaransa na Marekani kusaidia kupambana na waasi ili mazungumzo yaweze kufanyika. Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma tangu kuanza kwa uasi bwana Bozize aliwashutumu waasi kwa kupanga njama dhidi ya serikali na kuungwa mkono na kundi la upinzani wa kisiasa. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema waasi wana silaha za kutosha lakini chanzo cha namna wanavyopata msaada wao wa kifedha hakijulikani.

Pia Alhamis, Marekani ilifunga kwa muda ubalozi wake mdogo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwaondoa wafanyakazi wake kwa sababu ya kitisho cha uasi cha kuiangusha serikali. Washington inavisihi vyama vyote kuanza mazungumzo ya amani.

Umoja wa Mataifa umewaondoa wafanyakazi wake wa muda kutoka nchi hiyo kwa sababu ya kitisho cha ghasia.

Wapiganaji waasi wanasema hawana mipango ya kuuteka mji mkuu lakini hawata kaa kimya kama majeshi ya serikali yanachukua hatua yoyote dhidi yao.
XS
SM
MD
LG